KANUNI ZA MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI (Tangazo la Serikali Na. 249 la mwaka 2025)
Abstract
Uchaguzi wa haki, huru, amani na wa kuaminika hutegemea ushirikiano na uadilifu wa wadau muhimu wa uchaguzi katika kutekeleza wajibu wao wakati wa kuendesha kampeni na zoezi la uchaguzi. Kwa kuzingatia kifungu cha 162 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushauriana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyama vyote vya siasa imeandaa Kanuni za Maadili ya Uchaguzi kwa lengo la kuweka msingi unaopaswa kuzingatiwa na washiriki wa uchaguzi pamoja na hatua za kinidhamu zinazoweza kuchukuliwa kwa atakayekiuka Kanuni hizi.
Collections
- Subsidiary Legislation [189]