SHERIA YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI NA. 1 YA MWAKA 2024
Abstract
Sheria inayoweka masharti ya kusimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, kufuta Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, 1985 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, 1979 na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, na itaanza kutumika katika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika Gazeti la Serikali.