Show simple item record

dc.contributor.authorMKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, PRISCA J. ULOMI
dc.contributor.authorMKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, PRISCA J. ULOMI
dc.date.accessioned2023-09-20T09:51:56Z
dc.date.available2023-09-20T09:51:56Z
dc.date.issued2023-09-13
dc.identifier.citation“Vile mnavyoitetea Serikali na kushinda kwenye kesi zile ambazo Serikali ilikuwa na haki zile fedha ndiyo zinasaidia kuleta maendeleo ambapo tunajenga barabara, vituo vya afya, n.k. Ofisi hii ni muhimu ndiyo maana imekuwa Ofisi maalum. Ofisi hii ya Wakili wa Serikali kama vile tunavyofahamu wale Mawakili wengine wanalinda na kutetea maslahi iwe ni ya taasisi au ya mtu mmoja, sasa yeye ni Wakili Mkuu wa Serikali,” amesisitiza Balozi Dkt. Pindi Chanaen_US
dc.identifier.urihttp://localhost/handle/123456789/1301
dc.descriptionAkitoa taarifa kwa niaba ya OWMS, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende amesema kuwa OWMS ina jukumu la kuendesha mashauri mbalimbali ya madai na usuluhishi ndani na nje ya nchi kwa niaba ya Serikali na taasisi zake. Aliongezea kuwa OWMS pia inashiriki kuendesha mashauri yanayohusu Makampuni ambayo Serikali ina hisa, kwa mfano hivi karibu imeendesha shauri la benki ya CRDB lenye thamani yashilingi bilioni 33. Dkt. Luhende ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake OWMS imeweza kumaliza mashauri mbalimbali kwa njia ya majadiliano, ikiwamo shauri lililohusu ujenzi wa SGR lililofunguliwa nchini Rwanda. Pia, OWMS imeendesha shauri lililofunguliwa Baraza la Usuluhishi la London ambapo Serikali ilikuwa inadaiwa shilingi trilioni saba na kufanikiwa kumaliza shauri hilo kwa majadiliano. Hivyo, kuwezesha Serikali kuepuka kulipa fedha hizo. Amesema kuwa pamoja na OWMS kushinda katika kuendesha kesi na mashauri kwamajadiliano nje ya mahakama, OWMS imekuwa inakabiliana na changamoto mbali mbali kama vile baadhi ya taasisi za Serikali kuvunja mikataba au makubaliano ya kisheria waliyoingia na mtoa huduma au mkandarasi bila kuishirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivyo kuzalisha migogoro inayokiuka sheria za mikataba, baadhi ya taasisi za Serikali zinachelewesha malipo ya huduma kwa wakandarasi hivyo kupelekea kufunguliwa kwa mashauri ya madai dhidi ya Serikali ambapo miradi hiyo ingesimamiwa vizuri ingeepuka milolongo ya kuiingiza Serikali katika madai na migogoro isiyoisha na baadhi ya taasisi kutokutoa au kutoa ushirikiano hafifu wakati wa kuandaa nyaraka mbalimbali zinazohitajika mahakamani na usimamizi hafifu wa miradi hasa miradi ya ujenzi ambayo imepelekea kuleta migogoro inayoenda kwenye suala la usuluhishien_US
dc.description.abstractMhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa lengo la ziara yake ya kutembelea OWMS ni kufahamu majukumu yao na kujenga uelewa kuhusu namna wanavyotekeleza majukumu hayo ili taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ziweze kushirikiana kuhudumia wananchi kwa kuhakikisha nchi inazingatia misingi ya haki na utawala bora ili taifa la Tanzania liendelee kuwa taifa la amani. Pia, ameipongeza OWMS kwa kulinda haki na maslahi ya Serikali yasipokonywe ndani na nje ya nchi kwa kushinda kesi ambazo Serikali ilikuwa na haki na kuwa mabingwa katika kutetea vyema Serikali. “Vile mnavyoitetea Serikali na kushinda kwenye kesi zile ambazo Serikali ilikuwa na haki zile fedha ndiyo zinasaidia kuleta maendeleo ambapo tunajenga barabara, vituo vya afya, n.k. Ofisi hii ni muhimu ndiyo maana imekuwa Ofisi maalum. Ofisi hii ya Wakili wa Serikali kama vile tunavyofahamu wale Mawakili wengine wanalinda na kutetea maslahi iwe ni ya taasisi au ya mtu mmoja, sasa yeye ni Wakili Mkuu wa Serikali,” amesisitiza Balozi Dkt. Pindi Chanaen_US
dc.publisherOFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALIen_US
dc.subjectDAR ES SALAAMen_US
dc.titleMHE. BALOZI DKT. PINDI HAZARA CHANA AIPONGEZA OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI KWA KULINDA MASLAHI YA SERIKALI NDANI NA NJE YA NCHIen_US
dc.typeArticleen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record